Wakati leo Tanzania inasherehekea miaka 51 ya Uhuru wake, jiji la Mwanza linashuhudia safari ya treni ya kwanza ya abiria ikiwasili jijini hapa kutokea kituo cha kwanza jijini Dar es salaam, tangu mara ya mwisho ilipositishwa takribani miaka mitatu iliyopita kutokana na wawekezaji waliopewa dhamana kipindi hicho kushindwa kuliendesha shirika la utoaji huduma hiyo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk Charles Tizeba akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kwa maswali waliyokuwa wakiuliza sambamba na wananchi waliokuwa karibu kwenye kituo hiki cha reli jijini Mwanza hii leo kushuhudia kuwasili kwa treni hiyo ya abiria yenye mabehewa sita ya daraja la tatu na behewa moja kwa daraja la kwanza.
|
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk Charles Tizeba ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kuipokea treni hiyo alipata fursa ya kuzibainisha taratibu mbalimbali pamoja na Changamoto zilizopo...
|
Waandishi wa habari wakizinasa pointi... Kabla ya shirika la Reli nchini kubinafsishwa kulikuwa na safari za treni 4 zilizokuwa zikisafiri kwa kati ya Dar na Mwanza kila wiki, lakini lakini TRC ilipobinafsishwa idadi ya safari za treni ilipungua hadi kufikia 2, na ilipofika 2009 mwezi disemba safari zikafutwa kabisa.
Ni mwisho wa safari na hapa abiria akikusanya vyake kutoka kwenye chumba cha usafiri wa treni daraja la kwanza kupitia treni ya abiria ya kwanza tangu kusitishwa kwa safari zake miaka mitatu iliyopita Dar to Mwanza. |
magnificent points altogether, you simply gained a brand new
ReplyDeletereader.
What would you recommend about your post that
you made a few days ago? Any positive?
Look at my web site ; sponter.com