Hapa ni wakati Miyayusho akiingia ukumbini hapo kupanda ulingoni kwa ajili ya kuanza pambano hilo.
Hapa ni wakati Nassib, akiingia ukumbini hapo kupanda ulingoni kwa ajili ya kuanza pambano hilo.
Bondia, Francis Miyayusho (kulia) akimsukumia konde zito mpinzani wake, Nassib Ramadhan, wakati wa pambano hilo, lililoishia raundi ya 10, kati ya 12 baada ya Nassib kushindwa kuendelea na pambano kwa kuzidiwa.
Miyayusho (kushoto) akipanga ashambulizi.
Miyayusho (kulia) akichapana na Nassib.
Hapa, Nassib akijihami kwa kumkumbatia Miyayusho ili kupunguza kasi ya mashambulizi, jambo ambalo lilimfanya mwamuzi wa mchezo huo kumkata pointi kutokana na kukumbatia kila mara.
Ohooooh!!! Kushney, ''Nasikia Kizungu zungu kichwa kinaniuma'', Nassib alisikiza akimwambia msimamizi wake, huku akihesabiwa na mwamuzi wa mchezo huo.
Mashabiki wa mchezo wa ngumi wakifuatilia ndonga hizo zilizokuwa zikiendelea uliongoni.
Mashabiki wakimnyanyua juu Miyayusho, na kushangilia baada ya kutangazwa mshindi katika pambano hilo.
Miyayusho akishangilia ushindi huo na mashabiki wake huku akiwa na mikanda yote miwili aliyokabidhiwa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na michezo, Dkt. Fenella Mukangara, (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (wa pili kulia) Ben Kisaka na Mratibu wa pambano hilo, Bawazir, wakiwa meza kuu wakishuhudia ndonga hizo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, akimvisha mkanda wa Ubingwa WBF, Francis Miyayusho, baada ya kumtwanga kwa KO, mpinzani wake Nassib Ramadhan, katika pambano lao la kugombea ubingwa huo lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Saalaam. Miyayusho alishinda kwa KO katika rauindi ya 10 kati ya 12 za mchezo huo. Kushoto ni mratibu wa oambano hilo, Bawazir. Picha zote na Muhidini Sufiani
No comments:
Post a Comment