Kocha Kim Poulsen amekiri kuwa Stars kuweka kambi yake jijini Mwanza hakika lilikuwa ni wazo sahihi kwani hamasa imeongeza kwa wachezaji wake na hata walimu nao wanaahidi kuhakikisha wanacheza kufa na kupona kwenye michuano hiyo kwa nia ya kuiletea sifa nchi ya Tanzania. Haya yamejiri kwenye hafla ya kuwaaga wachezaji wa kikosi chetu kinachoelekea Kampala nchini Uganda hapo kesho.
Wachezaji a timu ya Taifa Tanzania bara pamoja na viongozi wakijadiliana na mastori kwenye hafla ya kuwaaga wachezaji wa kikosi kinachoelekea Kampala nchini Uganda hapo kesho..
|
Baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro Stars na viongozi wa soka Mwanza. |
Hewa safi ya Hoteli Tilapia....na kuchati kwa chati.... |
Refreshment kandokando ya ziwa Victoria |
Fun |
Yes we are... |
Picha ya pamoja kati ya Kilimanjaro Stars na viongozi wa soka mkoa wa Mwanza MZFA
|
WAKATI huo huo chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kimewataka mashabiki wanaohitaji kwenda kuishangilia na kuipa hamasa timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars inayoshiriki michuano ya CECAFA Challenge Cup 2012 inayotaraji kuanza jumamosi ya Novemba 24 mwaka huu Jijini Kampala nchini Uganda kujitokeza kwa wingi na kuonana na uongozi wa MZFA kwaajili ya taratibu za safari.
Kwa mujibu wa Katibu wa MZFA Bw.Nasbu Mabourk amesema kuwa maandalizi ya taratibu za kupeleka washabiki nchini Uganda kuishangilia Kilimanjaro stars katika kila mechi itakazocheza zimekwisha kamilika na kuahidi kutoa gharama halisi ya kwenda nchini humo siku ya ijumaa, ikiwa ni pamoja na ile ya hati ndogo ya kusafilia toka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza zitakazoratibiwa na MZFA kwa ajili ya kuwarahisishia mashabiki na kuwaondolea usumbufu.
No comments:
Post a Comment