Serikali ya kikoloni ya Uingereza ilihimiza sana raia wake wahamie katika nchi mabalimbali ambazo nchi hiyo ilikuwa inazitawala. Na kwa waliokubali kufanya hivyo, walipewa msaada maalumu "grants" kama mtaji wa kuwawezesha kuanzia maisha katika nchi hizo. Pia walihakikishiwa kupewa kipaumbele kwenye masuala yoyote ikiwa ni pamoja na kupewa ardhi yenye rutuba ambayo iliporwa kutoka kwa wenyeji wa nchi hizo.
Mojawapo wa nchi wahanga wa sera hiyo ya uingereza ni South Rhodesia ambayo baadaye ikawa Zimbabwe. Wakati wa uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980, wapigania uhuru wa nchi hiyo wakiongozwa na komredi Robert "mbabe" Mugabe, waliidai ardhi yao kutoka kwa walowezi ambayo mababu zao waliporwa. Serikali ya uingereza ikawaomba wapigania uhuru hao wawape miaka 20 wale walowezi, halafu baada ya hapo serikali ya uingereza ingewalipa fidia walowezi wale na kuiacha ardhi waliyokuwa wanaimliki.
Miaka 20 baada ya uhuru wa Zimbabwe, yaani mwaka 2000, wapigania uhuru wa Zimbabwe wakaikumbusha serikali ya uingerza kutimiza makubaliano yao ya 1980. Uingereza ikakataa, wapigania uhuru wakawa hawana namna zaidi ya kuitwaa ardhi ya mababu zao kwa nguvu.
Walowezi wakiongozwa na Uingereza na nchi nyingine za magharibi, wakaanza kumuandama Robert Mugabe na kumuwekea vikwazo ambavyo vimevuruga kabisa uchumi wa nchi hiyo.
MATOKEO YAKE SARAFU YA ZIMBABWE IMEPOROMOKA THAMANI KUPITA MAELEZO1
No comments:
Post a Comment