Friday, April 20, 2012

AY APAGAWA NA UKARIMU WA SUDANI KUSINI, ASEMA PAMOJA NA KUWEPO KWA VITA ALIWEZA KUFANYA SHOO KALI:


Post ya AY kwenye FB akiwa nchini Sudani Kusini.

Baada ya kurudi Bongo akitokea Sudani Kusini alikokwenda kupiga show kwa mara ya kwanza japo wamekuwa wakimwalika toka zamani, AY amesema kwamba hakuwa na hofu yoyote kwenda kwenye hiyo nchi ambayo iko vitani. Amesema, "Ulinzi ulikuwa mzuri kwangu, nilikuwa nalindwa karibu na askari nane ambao wote wana AK 47 pamoja na convoy, nilikuwa nalindwa mimi pamoja na watu wangu wanne niliokwenda nao, tulikuwa tunalindwa mpaka usiku tunapokwenda kulala".

Baada ya kufanya shoo ya kwanza, AY amesema jamaa waliikubali sana ikabidi wamwalike kwenye shoo nyingine ya pili ambayo ingefanyika kesho yake lakini ikashindikana baada ya kupokea simu kutoka jeshini kwamba vita imeanza hivyo kila kitu kikasimama, simu zikakatwa network, umeme hakuna ndege za kivita zikasikika huku wanajeshi wakipita kwenda vitani.

AY alipiga shoo alhamisi iliyopita huko Juba-Sudani Kusini ambapo baada ya shoo ya pili ya pili kufutwa, jamaa wakamkabidhi mkwanja wake na kesho yake asubuhi wakamsindikiza mpaka airport lakini wamemualika tena kwenye shoo nyingine mbili ikiwemo moja miezi minne ijayo katika sherehe za uhuru ambazo zimeandaliwa na serikali.

Kwa furaha AY amesema, "moja kati ya vitu nilivyokutana navyo vikanishangaza ni pale ambapo nilikuwa nakula usiku likapita kundi la wanajeshi halafu wakasema wewe ni AY wewe tunakujua wewe, hata aliyenipeleka Sudani alishangaa. Wale wanajeshi wakaniuliza tena wapi MwanaFaa wakimaanisha MwanaFA, nikasema aaaah..!! kumbe hata mgosi wanamtambua. Kingine ambacho kimenishangaza zaidi ni kwamba hela yao ina thamani kubwa kuliko hela ya nchi yoyote Afrika Mashariki".

No comments:

Post a Comment