Friday, April 20, 2012

KIFO CHA KANUMBA:RAY ALIA NA MANGE KIMAMBI BAADA YA "KUMCHAFUA'' KWENYE BLOG YAKE YA U-TURN:

Mwigizaji-Vincent 'Ray' Kigosi.

Baada ya stori kuenea kwamba mwigizaji Ray anahusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, mwigizaji huyo amezungumza exclusively kwenye 'Ampliya ya Clouds Fm'.  Amesema "nimekuwa nikizisikia sana hizi tuhuma, sio kweli kwa sababu Kanumba alikuwa mdogo wangu wa karibu sana tumetoka mbali sana kimaisha mimi na yeye, nimekuwa na mazoea ya kuona vitu kila siku vinaandikwa ambapo juzi nilipigiwa simu na kuambiwa nitazame kwenye blog ya U-turn ambayo anaimiliki huyu dada ambaye simfahamu anaitwa Mange Kimambi". Alikuwa ameandika kwamba amepata taarifa kutoka kwa polisi mmoja wa Oysterbay kwamba Ray ndiyo aliyepiga simu kwa Lulu siku ya kifo cha Kanumba kwa hiyo Lulu ametumika kufanya mauaji bila kujijua na pia kukawa kuna swali kwamba kwa nini Ray alikiuwa wa kwanza kufika kwa marehemu Kanumba, Mungu ndiye anayejua"-Ray.

Kwenye sentensi nyingine, Ray amesema kwamba, "kwa hiyo nataka kuwadhihirishia watanzania kwamba Ray ndiyo anahusika na hicho kifo, baada ya hilo nimeshirikiana na polisi na kushitaki na kufungua kesi ambapo hivi sasa ninapozungumza yupo polisi Oysterbay akihojiwa kwa sababu ameandika kitu ambacho kipo ndani ya uchunguzi, hana uhakika nacho sijui Lulu amekamatwa Coco beach, which is not true, sijui hizi habari kazipata wapi."

Akionesha kuumizwa, Ray aliongeza kwamba, "sasa hii ni kutaka kunivunjia heshima, mimi nafanya kazi ya kuigiza ndiyo maisha yangu unapoandika kitu kama hicho kwenye internet inafika sehemu kubwa dunia nzima sasa unategemea watu wanichukuliaje kama siyo kunivunia heshima, kunipotezea mashabiki wangu. Nasema hili sitoweza kuliacha, nitalifanyia kazi na nitalifikisha mahakamani ili iwe fundisho, sitolichekea".

Kwenye sentensi nyingine Ray ameamplfy baadhi ya maoni yaliyotolewa na watu mbalimbali kwenye hiyo habari iliyoandikwa kwenye hiyo blog. Amesema, "maoni niliyoyasoma mengine yanamwambia yule dada anachokiandika kinaweza kumcost kwenye maisha yake, na nyingine zinasema kwamba tuko tayari kumvamia Ray na kumuua, sasa hii kitu ni hatari sana kwenye maisha yangu kwa hiyo nimemshitaki polisi na kuandika kwa kusema chochote kitakachonikuta hata nikipigwa jiwe na kuanguka mimi nadili na huyo mwanamke kwa sababu yeye ndiye mtu aliyepublish hivyo vitu watu wanichukulie mimi vinginevyo kabisa tofauti jinsi nilivyo na sihusiki kabisa na hicho kifo. Kimsingi maisha yangu yapo hatarini lakini nasema haya maisha na nitaendelea kuvumilia."
SOURCE: Amplifaya/Clouds Fm:

2 comments: