Sunday, March 18, 2012

LADY JAY DEE: HUYU DADA NI MWIZI KWELI KWELI:


Huyu mnaemuona kajisikitisha hapa, ni mwizi kweli kweli
--
Huyu dada ni mwizi na amekiri mwenyewe kwa maandishi na karatasi ninayo (hand writting mbovu kabisa). alidhani akisema atanirudishia vitu ndio sitampeleka Police.

Niliporudi nimekuta amepewa deiwaka ya kuwa anakuja na kusafisha nyumbani kwetu kisha anaenda.Ilikuwa ni kazi ya muda tu flani kwakuwa nyumba ilikuwa imekaa muda kidogo bila kugusa gusa

Ilimchukua zaidi ya siku 10 na hakuwa amemaliza hata vumbi la sitting room, nilichoona kafanya ni kufua mapazia tu Wakati mimi nikishinda nyumbani siku moja au 2, nyumba yote inaisha.

TATIZO:
Tatizo lilikuja nilipoamua kushinda nyumbani siku nzima ya Ijumaa nikaita na watu 2 waje kunisaidia kwakuwa niliamua Nyumba lazima iishe kufanyiwa usafi na kieleweke

Katika kupanga, nikagundua kuna vitu vingi sana vina miss, Zikiwemo school bags nilizoleta zawadi kwa ndugu na jamaa
Ambazo hata nilikuwa sijazibandua label

Nilipouliza jibu likawa, Sijui, sijui
Na nilipofika tu kutoka safari simu yangu ikaibiwa nyumbani...Tunaishi wawili, sidhani Gardner anaweza kunibia simu, Ili iweje??

Tukadhani tumeisahau hotel ambapo tulilala juzi yake
JB Bellmonte zamani Paradise hotel hata ukiacha nini, urudi baada ya mwezi unakuta wamekutunzia, haikuniingia akilini.

Kwakuwa wamekuwa wakitupigia simu mara kwa mara kama tuki check out halafu tukawa tumesahau either, Viatu, nguo au hata JEWELLERIES

Nikaamua nitumie u smart maana hata kama kuna panya, hawezi kula simu na kama ni ma bag basi ningekuta ameyatafuna hawezi kula bag 3 akamaliza ndani ya siku 2

Nikampigia simu G kumwambia simu ilipotea juzi na leo ma school bags nilizowaletea ndugu zawadi zilikuwa 4, imebaki moja na huyu dada wa usafi anakataaa!!
Akaniambia mpe simu niongee nae
Nikamwambia dada shika simu yako
Sikujua alibanwa vipi ila akakubali ma bag kachukua na atayarudisha kesho yake, ila simu hajaiba Sikuamini Nikafunga mlango nikamwambia sasa naita Police Utatoa simu yangu na vitu vyote ulivyoiba Ama nakutandika mabao na nikitoka nakufungia humu ndani utalala wiki bila kula hadi useme vitu vyote ulivyoiba humu ndani

Baada ya saa nzima akakiri kuwa na simu kachukua Nikasema bado kuna vingine nakupa muda, kabla sijatoka humu ndani kwenda kwenye show nakupa pen na karatasi orodhesha vyote ulivyoniibia ....hakufanya hivyo Akasisitiza kuwa ataleta vyote kesho yake nimuachie aende na nisimpeleke Police. Ila akawa bado hajasema vyote ni nini na nini

Kuna taa nyekundu ina face mlango wa kuingilia ndani
Nikamwambia "Unaona kile kidude chekundu kinawaka pale juu"
Unajua ni nini?? Akajibu "HAPANA"

Nikamwambia hiyo ni Camera na ninao ushahidi wa vitu vyote ulivyochukua ila nilikuwa nataka ukiri mwenyewe, ndio nitajua umejutia kosa na kwamba hutarudia tena
Huwezi amini aliniorodheshea vitu alivyoiba kwenye karatasi, mpaka nikadata angekaa zaidi ya mwezi huyu angebeba hadi makochi

Kafungua mpk handbag yangu kaiba Dollar 100
Kakiri mpaka bureau alipoenda ku change Namanga kwa ushamba wake wakampa rate ya 130,000

Gardner alinipa dollar 400 nimshkie, kesho yake nikamuuliza ulinipa 3 au 4 akaniambia 4
nikamwambia haiwezekani ni 3, sasa hiyo 1 itajipeperishaje kutoka kwenye bag na lina zip, mpaka tukaishia tu kutokukubaliana yeye anasema alinipa 400 mi nabisha nasema alinipa 300....
Majibu yote yamepatikana baada ya kukamata mwizi

Mwizi anadai hiyo Dollar 100 aliiokota hakujua ni nini alipoenda kuuliza watu wakamwambia ni hela eti.
Nikamwambia utaokotaje kitu ndani kwa mtu na usimuulize ukaamua tu kuondoka nacho??

BAADA YA HAPO TUMEAMUA KUFUNGA CAMERA KWELI MAANA HILO NI FUNDISHO

Kwa sasa yuko mahabusu binti huyo anaeitwa FRIDA
Naskia pia aliiba na pale TIGO Tranic Plaza 40,000/=
Kwenye pochi ya mtu

Kabeba, nguo, viatu, simu, hela, hand bags zangu, school bags nilizoleta zawadi, video flip, n.k
Tunangoja akae selo mpaka ajikojolee na aseme vinginevyo ambavyo bado hajavitaja

BAADA YA HAPO MTANIELEWA KWANINI SIPENDAGI HAWA WATU NYUMBANI KWANGU.


Nikaja kugundua labda alikuwa anachelewesha kumaliza kazi makusudi, kwakuwa alikuwa analipwa kwa siku ili siku ziwe nyingi na mfuko utune, sikujali sana kuhusu hilo

No comments:

Post a Comment