Mtoto Cesilia Edward akiwa na Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Abdulkarimenzi za uhai wake.
--
Mtoto Cesilia Edward amefariki dunia saa tano usiku wa tarehe 08 katika hospitali ya Regency ya hapa jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amelazwa kwa siku mbili kwa ajili ya matibabu.
Marehemu Cesilia alikuwa na umri wa miaka 14 alikuwa na tatizo la moyo na figo kushindwa kufanya kazi na kusababisha tumbo kujaa maji na kuvimba aligundulika na tatizo hilo tangu alipozaliwa.
Kampuni ya Africa media Group wamiliki wa Channel ten Kupitia kipindi cha 'mimi na Tanzania' ilifanikiwa kumpeleka marehem Cesilia nchini India kwa matibabu mwaka 2011 mwezi Oktoba lakini hakufanikiwa kupata matibabu (operation) baada ya madaktari kuthibitisha kuwa alikuwa amechelewa kwa matibabu.
Cesilia alikuwa mtoto yatima na kulelewa na familia ya Bw. Peter Nyarugembe mkazi wa Mbagala kuu ambaye alikuwa akimlea baada ya kukuta akilelewa na dada yake wilayani Kisarawe na alimkuta na tatizo hilo ila kutokana na hali ya uchumi aliyonayo hakuweza kumsaidia kupona ugonjwa alionao na kuamua kuomba msaada kwa wasamalia wema kupitia Kipindi cha mimi na Tanzania.
Marehemu alifikishwa hospitali jumatatu ya tarehe 6 mwezi huu akiwa na hali mbaya iliyopelekea kupoteza fahamu na kumbukumbu kila wakati hali iliendelea hivyo mpaka umauti ulipomkuta. Mungua ailaze roho ya marehemu Cesilia mahala pema peponi Amen.
No comments:
Post a Comment