Friday, January 6, 2012

JE, WAJUWA; WANAUME MARUFUKU KUUZA CHUPI NA SIDIRIA NCHINI SAUDI ARABIA..?

Sheria mpya inayowapiga marufuku wanaume kuuza nguo za ndani za wanawake kama vile chupi na sidiria inaanza kutekelezwa hii leo nchini Saudi Arabia.

Wanaharakati wa kike katika Ufalme huo wa kiislamu wanatumai kuwa agizo hilo lililotolewa na mfalme Abdulla mwaka wa 2006, utamaliza mfadhaiko ulipo wakati wanawake wanauziwa nguo zao za wasaidizi wanaume madukani.


Ajira kwa wanawake:
Hatua hiyo itawapa fursa adimu zaidi ya wanawake 40,000 kuchukua nafasi za kazi zitakazoaachwa wazi.

Maafisa wa kidini wasiopendelea mabadiliko wamepinga vikali hatua hiyo ya wanawake kufanya kazi nje ya nyumba zao.

Serikali imepanga kupeleka waangalizi katika vituo vya biashara kote nchini kuhakikisha kwamba wasaidizi wanawake madukani hawabughudhiwi na maafisa wa polisi wa kidini.

No comments:

Post a Comment