Dada Evelyn Kaijage.
Ndugu zangu watanzania, chuo cha Westminster kilichopo katikati ya jiji la london, UK, kila mwaka kinatoa scholarship kwa watanzania kusoma degree ya kwanza na ya pili bure (Yaani unalipiwa ndege kwenda london na kurudi Tanzania, malazi, chakula, ada yote na pesa ya matumizi ambayo hutolewa kila mwezi).
Tatizo hizi habari tukipata hatupeani, mwisho nafasi kama hizi zinafutwa chuoni maana hamna wanaoziomba. Mi nilifanikiwa kuipata kupitia rafiki yangu, nami nimekuwa naitangaza na ntaendelea. Hii nafasi itasaidia kubadilisha maendeleo ya watanzania na Maisha yao kiujumla.
Link hiyo chini ina maelezo yote. Deadline ni mwakani April, so kama upo interested, tumia mda huu kudownload form za kuomba chuo, ukipata chuo, then unaomba scholarship, maelezo yapo kwenye website yao www.westminster.ac.uk link ni http://2009.westminster.ac.uk/study/international/country-pages/africa/tanzania
Goodluck
Evelyn Kaijage.
"Hasante sana dada Evelyn kwa kutuhabarisha maana si wengi wenye moyo kama huu. Mungu akubariki."
TAFADHALI MJULISHE NA MWENZIO UONAPO HABARI HII!
Caris Komba,
MD - Caris Blog
Hasanteni sana.
No comments:
Post a Comment