Tuesday, November 15, 2011

MAJI YALIVYOTEKETEZA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA BAADA YA MVUA KUBWA YA JANA, UWANJA ULIFUNGWA KWA MUDA, ABIRIA WASHINDWA KUSAFIRI:


Mvua kubwa iliyonyesha jana jijini Mwanza kwa takribani masaa manne imeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za usafiri na usafirishaji kwa njia ya anga.
kwasababu za kiusalama hakuna ndege iliyoruhusiwa kutoka au kuingia Air port Mwanza.
Hali ilikuwa mbaya zaidi majira ya saa mbili asubuhi ambapo maji mengi yaliyokuwa yakitiririka kutoka eneo la mwinuko kaskazini mwa kiwanja cha ndege Mwanza, yalisababisha taswira ya uwanja kubadilika na kuwa kama sehemu ya mto mkubwa unaotiririsha maji kuelekea ziwa victoria.
Pichani ni kama ndege iliyogota katikati ya shamba la mpunga kumbe laaa!! ni ndege iliyo katika eneo stahiki la maegesho ya ndege.
Wafanyakazi mbalimbali kiwanjani hapo wakishughulika kusafisha njia za ndege mara baada ya magugu na tope jingi kutanda eneo hilo.
Hawa ndege sijui walitoka wapi!!! Naskia ni hatari sana kwa ndege ndogo za abiria. Ndege hawa peke yao ndiyo walipata fursa ya kupaa lakini zile zingine za abiria kushnei....
Wafanyakazi wa idara tofauti kiwanjani hapo wakihaha kuzima swichi za umeme kiwanjani hapo mara baada ya kina cha maji kuanza kupanda taratibu kikitishia usalama.
Wafanyakazi sekta ya mizigo walifanya kazi ya ziada kunusuru mizigo ilokuwa tayari imepakiwa kitengo cha mizigo isilowe.
Pata picha kama ndege zingeruhusiwa kuondoka au kutua wakati wa mafuriko ile hali tayari njia za ndege zishaharibika, Si mchezo......!!!!!???!!.
Hapa unaambiwa ni hali imetulia kwa Ofisi zetu kiwanjani. Mara baada ya maji kupungua unaweza kuona jinsi miundo mbinu hasa njia za ndege ilivyoathirika. Chekshia ngazi za ndege....Kikazi zaidi...kama shambani vile.
Hali halisi....hatoki mtu haingii mtu...!!

No comments:

Post a Comment