Wednesday, August 3, 2011

SAKATA LA MGOMO WA VITUO VYA MAFUTA JIJINI MWANZA:

Hakuna hata gari moja.
Peupeeee peee. Ni kamba tu zimefungwa zikiashiria hakuna huduma mpaka kieleweke.
Tazama hiyo habari picha. Ni kituo cha mafuta cha GAPCO kilichopo katikati ya jiji la mwanza, mkabala/opposite na  kituo cha daladala almaarufu kwa jina la Kemondo, pia kituo hichi cha mafuta cha GAPCO kiko ubavuni mwa ofisi za benki kuu ya Tanzania tawi la Mwanza.

Mgomo huu wa kituo hichi ni moja tu kati ya vituo vingi vilivyogoma hapa nchini ikiwa ni shinikizo la kuipinga serikali kufuatia kauli yake ya kuvitaka vituo vyote vya mafuta nchini kushusha bei ya mafuta.

No comments:

Post a Comment