Mgunga (Production Director wa Parapanda) na Zodi (Costume Designer) akionesha kazi zake alizowahiku-design.
Mgunga Mwamnyenyelwa akiwatambulisha wasanii wa kundi la Parapanda kwa wasanii wa Sweden ambao kwa pamoja watashirikiana katika uigizaji wa tamthilia hiyo.
The production Directors: Mgunga Mwamnyenyelwa wa Parapanda (Kushoto) na Ronny Hallgren.
The Gothernburg City Theatre building.
Eva (Antigone) akiwa katika mazoezi (Rehearsal) kabla ya upigaji picha kuanza.
Men at work, The production Directors, wakiwa katika maandalizi wa muvi hiyo ya "Antigone".
Wasanii 7 na mwongozaji mmoja wa kundi la sanaa za maonyesho la Parapanda wako nchini Sweden kwa ziara ya maonyesho ya utambaji wa mashairi na uandaaji wa tamthiliya ya ANTIGONE. Tamthiliya hii imeandikwa miaka 42 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo, zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Mwandishi wake ni yule msanii na mwandishi nguli wa kigiriki wa tamthiliya za jukwaani aliyejulikana kwa jina la Sophocles.
Tamthiliya hii imetafsiriwa katika lugha zote kuu za dunia kasoro Kiswahili na kwa mara ya kwanza itachezwa kwa Kiswahili na Kiswidi.
Maandalizi na maonyesho ya tamthiliya hii yanafanywa na taasisi mbili za sanaa za maonyesho: Parapanda Theatre Lab Trust ya Tanzania na Gothernburg City Theatre ya Swideni kuanzia tarehe 2/8/2011 mpaka 14/12/2011. Maandalizi na maonyesho yanafanyika Swideni na Tanzania.
Majina ya Wasanii (Waigizaji) na Waongozaji.
Parapanda Gothernburg Theatre:Jane Mwatonoka Nina Zanjani
Frank Samatwa Johan Karlberg
Habiba Nguogani Fredrik Evers
Amani Lukuli Anna Bjelkured
Shabo Makota
Daudi Joseph
Eva Nyambe.
Waongozaji
Tamthliiya hii inaongozwa(directed) na Mtaalamu na muongozaji maarufu wa tamthilya za jukwaani Mgunga mwa Mnyenyelwa wa Parapanda Theatre na bwana Ronny Hallgren mwongozaji mashuhuri wa tamthliya nchini Swedeni. Bwana Ronny pia ni Mkurugenzi wa jumba la maonyesho la sanaa la jiji la Gothernburg.
Mahusiano:
Ushirikiano huu ulianza miaka takribani 10 iliyopita ikiwa ni matokeo ya mradi wa PACSEA ( Performing Arts Coorperation Between Sweden and East Africa) ambao ulikuwa ni ushirikiano baina ya Uswidi na nchi za Masharik mwa afrika; Kenya,Tanzania,Uganda na Ethiopia .( Mradi huu uliokuwa unaratibiwa na taasisi ya sanaa kusini mwa afrika –EATI kwa ufadhili mkubwa na SIDA, ulifikia kikomo mwaka 2009.
Wakati wa mradi huu vikundi na taasisi za sanaa za maonyesho kutoka nchi za mashariki mwa Afrika ziliweka urafiki na wasanii wa vikundi na taasisi za Uswidi. Katika Mahusiano hayo vikundi vilitembeleana,vikafanya warsha na kushiriki katika matamasha ya Uswidi na Tanzania.
Ni wakati huu ndipo taasisi ya sanaa ya Prapanda Theatre Lab Trust ilipopata rafiki kutoka Uswidi ambayo ni taasisi ya kuandaa na kuonyesha tamthiliya ya serikali ya jiji la Gothernburg kwa jina la Gothernburg City Theatre.
Ni wakati huu ndipo taasisi ya sanaa ya Prapanda Theatre Lab Trust ilipopata rafiki kutoka Uswidi ambayo ni taasisi ya kuandaa na kuonyesha tamthiliya ya serikali ya jiji la Gothernburg kwa jina la Gothernburg City Theatre.
Parapanda & Gothernburg City Theatre.
Chimbuko la mahusiano ya taasisi hizi mbili ni Tamasha la Sanaa la EATI lilifanyika Mombasa Kenya. Mkurugenzi wa GCT mr Ronnie Heglen alifika kutoka Swideni na kushuhudia onyesho la “Kalunde” ambalo lilikuwa ni mchanganyiko wa utambaji wa hadithi, muziki na ushairi. Uongozi wa kutoka Jumba la sanaa la Gothernburg ulikaa kikao na uongozi wa Parapanda chini ya bwana Mgunga Mwa Mnyenyelwa kuhusu nia ya kuanzisha ushirikiano wa kisanii.
Ushirikiano huu uliwasilishwa rasmi katika vikao vya PACSEA na EATI na kukubaliwa.
Hatua ya awali katika ushirikiano huo ika ni kuwa na warsha ya kutambuana na kubadilishana mawazo . Warsha hii ilifanyika mwaka 2005 katika ofisi za Parapanda. Wasanii sita kutoka GCT walikutana na wasanii nane wa Parapanda kwa muda wa wiki moja. Ni katika warsha hii ambapo wasanii wa Parapanda walionyesha hazina waliyonayo katika sanaa.Warsha kama hiyo ikafanyika mwaka 2008 nchini Uswidi. Halikadhalika huko wasanii wa Parapanda walijifunza mbinu na aina ya sanaa inayofanywa na GCT.
Wasanii wa Parapanda walishiriki katika matamasha ya Utambaji hadithi na ushairi nchini Swideni mara mbili; 2005 na 2007.Baada ya kufahamiana vizur,i Uamuzi wa kuandaa onyesho la pamoja ulifanyika. Mapendekezo yalitolewa na GCT kwamba tamthiliya ya Antigone ndiyo ingefaa kuandaliwa. Sababu kubwa ilikuwa; ni tamthiliya kongwe inayoheshimika duniani na pili ni tamthiliya inayoeleza masuala kadhaa ambayo yanaakisi maisha ya leo ya sehemu nyingi duniani ikiwemo Tanzania. Suala kubwa ni Harakati za Mwanamke kupambana na mifumo gandamizi, wajibu wa raia, migogoro ya kitabaka na kiutamadini na nafasi ya vijana katika jamii inajitokeza.
Uamuzi wa kuandaa tamthiliya hii ulikubaliwa na Parapanda na kuanza kuandaa ratiba ya utekelezaji . Kwa mujibu wa mradi huu, wasanii saba wa Parapanda na wanne wa GCT watachukua uhusika. Kutakuwa na waongozaji wawili, Mgunga Mwa Mnyenyelwa (Parapanda) na Ronnie Hegllen (GCT). Onyesho litatumia sehemu kubwa ya mbinu za uwasiishaji za Parapanda hususani katika muziki,ngoma na ushairi.
Wakati wa ziara hiyo Parapanda mealikwa kufanya maonyesho ya muziki na utambaji wa mashairi na ngoma katika tamasha la Utamaduni la watu wa Gothernburg wiki ijayo tarehe 19/8/2011 usiku katika uwanja maarufu wa maonyesho ya nje wa Gothernburg City . Makundi mbalimbali zaidi ya ishiriki kutoka ndani na nje ya Swideni yantarajiwa kushiriki. Wasanii wa Parapanda wapo katika mazoezi makali ya kushiriki tamasha hilo sambamba na maandalizi ya tamthliya ya Antigoni
Mgunga Mwa Mnyenyelwa
Mwongozaji &Mkuu wa msafara.
No comments:
Post a Comment