Fikiri ni mwanafunzi katika shule ya sekondari Mabadiliko. Yuko kidato cha pili.
Shule ya sekondari Mabadiliko imekuwa na uhaba wa walimu. Katika masomo tisa anayosoma Fikiri ni masomo matatu tu yenye walimu, ambayo ni hisabati, jiografia na kiswahili. Masomo haya pia yamepatiwa vitabu vya kutosha kwa sababu rasilimali zote za shule hiyo zinaelekzwa kwenye masomo hayo yenye walimu.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mabadiliko anategemea mwaka ujao wa fedha walimu watakubali kuja kufundisha shuleni hapo kwa kuwa tarafa yao kwa mara ya kwanza itapata nishati ya umeme. Vilevile tayari kijiji kimeshapatiwa kisima cha maji. Ukosefu wa maji na umeme uliwafanya walimu kukataa kabisa kupangiwa kazi katika shule ya Mabadiliko.
Fikiri amekuwa akirudia kidato cha pili kwa miaka miwili sasa. Ameshindwa kupata alama za wastani wa kumuwezesha kuingia kidato cha tatu. Wanafunzi wengine wamefanikiwa kupata alama hizo na wanaendelea katika vidato vya juu.
Wazee wa kijiji wanafahamu kuwa Fikiri hatilii maanani masomo yake. hivyo waliamua kumuweka chini na kumhoji. Alipoulizwa sababu za kushindw kupata wastani wa kuendelea kidato cha tatu, Fikiri alisema kuwa swali hilo linamtia hasira. Amesema hali ya shule yao kukosa walimu kila mtu anaifahamu na kwanini washangae yeye kukosa wastani wa kufaulu. Katika mitihani yake Fikiri hupata F za masomo nane na D ya somo la Kiingereza.
Tangu kipindi hicho Fikiri amejenga chuki na wazee wa kijiji cha Mabadiliko na amekuwa akilaani kitendo chao cha kumuona yeye mzembe wakati wanajua hali ya uhaba wa walimu ilivyo. Fikiri amejitoa katika kushiriki shughuli za maendeleo kijijini na marafiki zake wengi amegombana nao.
Somo: Pamoja na shule ya mabadiliko kukosa walimu wa masomo mengine, lakini uwepo wa walimu wa Hisabati, jiografia na kiswahili ulipaswa kutumiwa ipasavyo na Fikiri katika kujiendeleza kimasomo na kupata wastani wa kuendelea vidato vya juu.
Fikiri alitoa kipaumbele zaidi kwenye kulalamikia udhaifu uliopo ambao kwa kiasi kikubwa uko nje ya uwezo wake kuutatua badala ya kuzingatia zaidi nafasi yake katika kutekeleza wajibu wake.
Je, walimu wa masomo mengine wakiripoti Fikiri atabadilisha tabia yake na kuanza kufanya bidii? au tabia hiyo itakuwa ndio mfumo wake wa maisha na atakachofanya ni kutafuta sababu nyingine ya kulalamika?
COMMENTS/MAONI MBALIMBALI:
1: Ni darasa nzuri. Ninamuona Fikiri kama mwakilishi wa Watanzania wengi ambao huficha udhaifu wao katika mapungufu ya serikali na nchi.
Kwa sababu hatuna mfumo wa uwagiliaji maji na vifaa vya kisasa vya kilimo na uvuvi, tunaacha kulima na kuvua kwa kutumia vile tulivyonavyo, badala yake tunakaa vijiweni kukosoa na kusubiri serikali ifanye...ifanye hata kutengeneza madawati na vikalio wakati tumezungukwa na misitu, ifanye hata kufyeka pori, ifanye hata kusafisha uwanja wa nyumba yetu seuze mtaro unaopita kijijini petu.
Kwa kuwa Fikiri ni mtu wa kusubiri kufanyiwa, ataendelea kulalamika hata baada ya kila kitu kuwepo.
2: Sawasawa,
Kwa hiyo in summary tunaweza kusema "if you play your part and I play my part, it can be done". Hakuna viwanda au shule ya viongozi. Viongozi ni miongoni mwa wanajamii. Yale yanayofanywa na mwanajamii leo ndio atakayofanya akiwa kiongozi. je, mwanajamii anaonyesha dalili za kuwa kiongozi mzuri? je, anajali maslahi ya umma kivitendo? Je anatoa taarifa za uhalifu wote anaoushuhudia? Je, ana uchungu na nchi yake? kama mwanajamii wa kawaida hana hivi na jamii inaona hilo ni jambo la kawaida, basi tusitegemee hayo kwa viongozi hata kidogo.
3: Tatizo letu ni kuwa system tuliyonayo imeoza. Kwa sisi tuliozaliwa na kukulia ndani ya enzi ya ujamaa (pamoja na mapungufu yake) tulikuwa tunagawana umasikini wetu na tunaridhika na tulichonacho, kiasi ikafika wakati kila mwananchi anajiona sehemu ya taifa, analinda mali ya taifa. Ni kweli walikuwepo wakorofi wachache lakini walikwa wanahesabika. Miradi mingi iliyoanzishwa ilikuwa nguvu za wananchi wenyewe kwa hivyo waliitumikia na kuilinda, leo unamhamisha mwananchi kwa nguvu, bila ya kumtafutia pengine wala kumlipa fidia, fedha zilizotengwa kulipia fidia zinaishia mikononi mwa wajanja na wanasiasa walafi, unatarajia wananchi wataulinda mradi huo?
Lilipokuja suala la kukaza mkanda tulikaza wote, watoto wa viongozi walisoma nchini, baba zao tulikuwa tunapigana na vikumbo kwenye foleni za kilo ya unga na sukari na hospitali, wabunge walikuwa wakienda Dodoma ndani ya basi moja, leo wanadiriki hadi kupanda ndege. Leo hakuna nyongeza ya mshahara wa mwalimu, daktari, polisi, bwanashamba, lakini za kuwaongezea mishahara na posho wabunge pamoja na kuwapa kiinua mgongo cha maisha yao zipo. Leo watoto wao wanasoma nje au kwenye Internationals, wetu wanagaragara kwenye vumbi, wao wakishikwa na homa wanatibiwa nje, sisi tunalala hospitali mpaka kwenye sakafu. Na ndio maana uzalendo umepotea, sasa takriban sote tumekuwa wakorofi kwa sababu mfumo umetufanya tuwe hivyo.
Mwanajamii anaweza kuwa kiongozi mzuri ikiwa alipata kuongozwa na kiongozi mzuri. Nadra kwa leo kupata kiongozi mzuri kutoka miongoni mwa wanajamii wakati yeye aliongozwa na kiongozi mbinafsi, mhujumu wa mali ya umma na mbinafsi.
Fikiri ni zao la mfumo wetu, hivyo usitarajie kuwa Fikiri atakuja kuwa kiongozi mwema.
4: Ninachoona ni jamii kujiadhibu yenyewe.
Katika saikolojia tunafundishwa jambo likisemwa vizuri, basi huwa linapendwa kufanywa na wengi. Mtoto akisikia kufaulu kunasemwa vizuri basi atajitahidi afaulu.
Jamii yetu ilikuwa na viongozi wazuri. Lakini kwa vile nchi yenyewe bado uchumi wake unachechemea na mfumo wa mafao uko dhaifu, viongozi hao wazuri walipostaafu hali zao kimaisha zilibadirika na kuishi maisha ya chini. Kukawa na baadhi "wakorofi" ambao walifanya ubadhilifu na walipostaafu wakaendelea kuishi maisha mazuri pengine zaidi ya wakati wakiwa madarakani.
Wale viongozi waadilifu wanasemwa na jamii kuwa "wamechezea nafasi". na wale wabadhilifu wanapongezwa kuwa "watu wa deal". Juzi ulipotokea msiba wa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo mama Hawa Ngurume, tuliona watu wakidhihaki hali ya mama yake mzazi kuwa na nyumba inayofanana na wanakijiji wengine. Ilisemwa kuwa mama Ngurume R.I.P amechezea nafasi badala ya kujiimarisha kiuchumi. Kwa anayeifahamu kazi ya ukuu wa wilaya na mafao yake anajua wazi kuwa ukuu wa wilaya haumuwezeshi mtu kuwa tajiri iwapo atakuwa mwadilifu. Kwa hiyo kilichosemwa ni kwamba mama Ngurume amefanya kosa kutokuwa mbadhilifu.
Hivi ndivyo jamii inavyojiadhibu.
Kuna wanaoanza kuamini labda kuna chama cha siasa kinaweza kubadilisha hali tuliyo nayo. Lakini sijafanikiwa kumpata mtu anayeelezea jinsi chama cha siasa kinavyoweza kubadilisha hali hii, kwa sababu misingi yake ni kuanzia kwenye familia.
Kuna vijana wengi nimewakuta Marekani hawataki kujenga nyumbani ingawa wana kipato cha kutosha kujenga na wanapenda kujenga. Sababu wanayonipa ni kwamba experience inaonyesha waliojaribu kujenga wakiwa mbali asilimia kubwa ya pesa walizotuma zilitumiwa tofauti na madhumuni - ufisadi at family level. Hii ndio kama yale masomo ya kiswahili, hisabati na jiografia ambayo Fikiri ana mwalimu lakini anashindwa kujitahidi. Je, at family level nayo tutailaumu serikali? Kama system mbovu at least tujenge jamii ya uaminifu at family level...
5: To greed, all nature is insufficient.

No comments:
Post a Comment