Wadau na sinema za RJ Company napenda kuwafahamisha kuwa nimeamua kutoa movie hii ya The Glory of Ramadhani kwa ajili ya mwezi mtukufu unaokuja hivi karibuni , lengo ni kufikisha ujumbe kwa ndugu zangu Waislam kwani si waislam wote wanaenda misikitini kusikiliza mawaidha basi kupitia sinema hii watu watajifunza mambo mazuri ya kumpendeza Mungu hii si ya kuikosa, maasusi kwa mwezi mtukufu lini itatoka? ni kabla ya siku tatu kuingia kwa Ramadhani..
Huu ndio mwanzo wa The Groly of Ramadhani ni filamu ambayo tuliweza kuifanya kwa umakini mkubwa sana ili watu wajifunze kutenda mema kwa miezi yote kumi na mbili na si mwezi mmoja..
Kazi imeanza..
The Greatest nikiwa na vijana wangu kazini.
Mambo yakiendelea kupamba moto wadau huu ni mzigo hatari wenye mafunzo ya kutosha.
Chuchu Hans on set.
Chuchu Hans pamoja na Dura wa kipindi cha Planet Bongo wakiwa on set huku The Greatest nikiwapa maelekezo jinsi scene inavyotakiwa kuchezwa, wadau huyu kijana Dura ni tunda la baadaye litakalokuwa bora kwa miaka ijayo kama unabisha nunua mzigo huu utaamini nachokisema
Angalieni vijana wanavyofanya kazi.
Chuchu Hans akiwa na Dulla kijana huyu anakuja vizuri anaweza kuja kuwa Kanumba wa baadaye.
Kazi ikifanyika.
Tukiwa nje ya mji.
Mimi sisemi cheki mwenyewe watu walivyo makini na kazi zao hii ni moja ya scene ambazo watu wengi waliikimbilia kwa ajili ya futari sikupata tabu sana kupata exttra..
The Greatest nikiwa na Neshi katika The Groly of Ramadhani wadau nimetimiza yale mliokuwa mkiniambia kuhusu huyu dada kuwa mnahitaji nicheze naye sinema haya bila nyinyi mimi nisingefika hapa hivyo sina budi kuwasikiliza katika mambo mazuri mnayoniwazisha.
Neshi na Bachard.
Neshi akikamua.
The Greatest na Nesh on set tukifanya vitu
Hii ni scene ambayo ilikuwa ngumu sana kuitengeneza..
Kila jambo lina wakati na huu ni wakati wa The Glory of Ramadhani.
Tuliweza kupata location zenyewe kama mnavyotuona.
Asante Mungu kwa kunitia nguvu kwa kuweza kuendelea kuelimisha jamii kwani Mungu baba hii ni kazi ulionichagulia mwenyewe na ndio maana unabariki kazi ya mikono yangu.
No comments:
Post a Comment