Saturday, July 14, 2012

JINSI JOSSE CHAMELEONE ANAVYO-MAKE MORE MONEY:


Baada ya kukutana na staa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone nimegundua kuna mambo mengi nilikua nayasikia tofauti na kuyasoma ambayo yeye ameyazungumza tofauti kabisa.
Nilikua sijui, kumbe Chameleone alianza kuenjoy kuwa staa kuanzia mwaka 2000 japo alianza muziki 1995, 2003/2004 ndio alianza kupata pesa na hapo ndipo maajabu yalianza kutokea kwa kuanza kutimiza ndoto.
Millard Ayo na Jose Chameleone.
Chameleone amesema “nilijenga nyumba yangu kwa miaka miwili ambapo 2005 ilimalizika na ikawa imegharimu shilingi milioni 200 -300 za kitanzania, wakati nilikua naijenga hiyo ndio pesa niliyokua nayo na nikasema kabla sijaipoteza acha nifanye kitu muhimu lakini Mungu akanibariki tena baada ya kujenga hiyo nyumba nikapata bahati nyingine nikaendelea na vitu vingine”
Jose Chameleone (katikati) akiwa kwenye shooting ya moja ya video zake.
Exclusive na millardayo.com Mwimbaji huyu staa kutoka Uganda amesema vyanzo vyake vikubwa vya mapato kwa sasa ni kununua na kuuza ardhi, kuuza simu za mkononi ziitwazo Chameleone anazozitengeza China, kununua nyumba na kuziuza pia kupangisha nyumba.
kuhusu vyanzo vingine vya mapato Chameleone amesema “show pia zinatulipa sana Uganda japo siwezi kukwambia nalipwa bei gani kwa sababu sipendi kuonekana mtu wa kujisifia lakini kwa wiki moja naweza kupiga show mbili Kampala au Uganda, na kingine kinachotulipa sana ni Kampuni kubwa za biashara ambazo zikikuona una nguvu zinakuchukua na kukulipa vizuri kwa kufanya nao promoshen au mambo mengine ya mkataba wa biashara”

No comments:

Post a Comment