Jacquline Wolper (Kulia) naye akitamba mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwa atamchana chana vibaya sana mpinzani wake Wema Sepetu katika tamasha la Matumaini litakalofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
"Sipendi maneno, napenda vitendo, nimekuwa nikisia Wema na rafiki yake wanaongea sana kwenye TV kuhusu mimi, nataka nikate mdomo wake siku hiyo kwa kumpiga", alisema Wolper.
Nahodha wa timu ya Bongo Flava akiahidi ushindi kwa timu yake dhidi ya Bongo Movie FC.
Kutoka kushoto: Kocha wa bondia Francis Cheka (Abdallah Saleh-Komando), Francis Cheka, meneja wa mfuko wa elimu (Charles Kapima), mmoja wa waratibu wa tamasha hilo (Luqman Maloto), promota wa pambano hilo, Kaike Silaju, bondia, Japhet Kaseba na mwisho ni meneja wa Kaseba, Idd Bakari.
Waandishi wa habari wakifuatilia hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment