Friday, April 13, 2012

KONGAMANO LA KIGODA CHA MWALIMU:

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakitoka baada ya kuhudhuria kongamano hilo.
  Mwandishi mkongwe,  Jenerali Ulimwengu akisoma kitabu cha Mwalimu Nyerere kwa washiriki wa Kongamano hilo.
 Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa (wa pili kulia), akimsikiliza mwandishi mkongwe Jenerali Ulimwengu wakati akipitia yaliyoandikwa kwenye kitabu cha Mwalimu Nyerere kabla ya kuzinduliwa katika Kongamano la nne la kitaaluma la Julius Nyerere lililofikia tamati Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mukandara (kushoto) akiwa na Profesa Issa Shivji.
 Waziri Mkuu wa zamani, Dk. Salim Ahmed Salim (kushoto) akiwa na akiwa na mwansiasa mkongwe, Joseph Butiku (kushoto kwake) wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano hilo.
Mwezeshaji wa Kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Micere Mugo (kulia), kutoka Kenya, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha  Mwalimu Nyerere kinachoelezea makala na hotuba zake katika Kongamano la nne la Kitaaluma la Julius Nyerere lililofikia tamati Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Nyerere, Profesa Issa Shivji.

No comments:

Post a Comment