Anaitwa Mariam Elias mwenye umri wa miaka 19, wazazi wake wanaishi vigwaza yeye anafanya kazi misugusugu ambapo kwa huzuni huku akiwa analia amesema “nilijisikia vibaya sana na ndio maana mpaka sasa hivi bado najisikia uchungu kwa sababu ni msanii ambae tulikua tumemzoea Tanzania tunapenda sana cd zake, kusema ukweli hamna msanii bongo ambae kwanza anapenda kuigiza sana na watoto, Uncle JJ, BIG DADDY kusema ukweli tulimzoea na mpaka sasa hivi siwezi kurudi tena misugusugu maana najisikia uchungu sana”
Kuhusu siku aliyokunywa sumu, Mariam ameamplfy kwamba “tulikua tunatazama taarifa ya habari saa mbili usiku kwenye TV, kusema kweli niliiangalia nusu na walivyomaliza sala ya mwisho nilijisikia vibaya nikazunguka zangu ndani nikaanza kulia, nililia sana kwa sababu toka msiba ulivyotokea nilikua bado nalia, nilivyonyamaza bado roho ikawa inaniuma sana nikachukua uamuzi wa kunywa sumu, ndani kulikua na shilingi 300 na kuna dada alikua karibu yangu nikachukua shilingi 200 nikaenda kununua sumu nikakoroga nikanywa lakini baada ya kunywa nikaona bado haijafanya kazi, ikabidi nichukue tena shilingi 200 nikaenda kununua nyingine”
Mariam ambae anafanya kazi ya kuuza vinywaji bar amesema “nilikua nataka kujiua na nilimwachia Mungu mwenyewe, kujiua kwangu kungepunguza mimi kumfikiria sana Kanumba, nimeanza kumfatilia toka nikiwa darasa la tano ambapo shule ya msingi nimemaliza 2007, tarehe 14 April 2012 natimiza umri wa miaka 20″
Baada ya kunywa sumu alianza kusikia tumbo likimuuma sana na kuongeza kwamba “kuna chumba cha huyo mama ninae kaa nae akaanza kuuliza nimefanyaje, lakini mtoto wake ambae alikua karibu yangu wakati nakunywa sumu ilibidi amwambie mama yake kuhusu nilichofanya, mama aliponiuliza kweli nikakubali ndio wakanipa huduma ya kwanza kwa kunipa maziwa na maji ya baridi, nikachukuliwa na gari mpaka hospitalini Tumbi”
Kwenye sentensi nyingine Mariam amesema “kusema kweli mimi niliwahi kufiwa na kaka yangu wa kwanza 2008 lakini huo msiba haukuniuma kama nilivyoumia kwa Steven Kanumba”
Kweli naamini ukiwa mtu wa watu watu watakupenda pole sana binti kwa kuwa na maamuzi yasiyokuwa na ushirikishwaji ila nakushauri uwe na moyo wa kupenda maisha yako kwani hujui saa wala sekunde ya Mungu kukuhitaji kwa nia iliyo salama!
ReplyDeletewww.ramsoict.blogspot.com
Kama kawa mzazi Ramso
ReplyDelete