Friday, March 30, 2012

ASKARI WA USALAMA BARABARANI MKOANI IRINGA WAMKAMATA ABIRIA WA BASI LA SUMRY NA VIPANDE 31 VYA PEMBE ZA NDOVU:

Mtuhumiwa aliyekutwa na vipande 31 vya pembe za Ndovu akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Sehemu ya askari polisi wakjadili jambo ya ulinzi wa polisi.

 Vipande 31 vya Pembe za Ndovu vilivyokuamatwa leo.
 Vipande hivyo vilihifadhiwa humu.

Wananchi na polisi wakiwa wamelizunguka basi la Sumry ambalo mtuhumiwa alikuwepo.
ASKARI wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Iringa kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji mkoa wa Iringa wamemkamata abiria Suleiman Amidu aliyekuwa akisafiri na basi la Sumry lenye namba za usajili T640 BEW Nisani ambalo lilikuwa likitoka mkoani Mbeya Dar es Salaam akiwa na vipande vya pembe za nduvu 31.

Abiria huyo alikamatwa leo majira ya saa 6 mchana katika eneo la Igumbilo katika manispaa ya Iringa ambalo ni eneo maalum kwa ukaguzi wa Mabai (check Point ) mkoani Iringa.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi abiria wa basi hilo la Sumry John Kyando na Sarah Sanga walisema kuwa abiria huyo mwenzao alipandia eneo la Stendi kuu ya Mbeya na kuwa alikuwa na mabegi matatu meusi ambayo yalionekana kumzidi nguvu ila hakutaka kusaidiwa na mtu yeyote .

Alisema Kyando kuwa kazi nzuri iliyofanywa na askari wa usalama barabarani mkoa wa Iringa na idara ya uhamiaji ndio ambayo imefanikisha kukamatwa kwa pembe hizo za ndovu na kuekeza masikitiko yake kwa askari wa usalama barabarani mkoa wa Mbeya ambao wameshindwa kubaini mzigo huo.

Kwani alisema kuwa iwapo askari wote wa usalama barabara wangefanya kazi kama askari wa mkoa wa Iringa vitendo vya vya ujangili katika hifadhi za Taifa na waharifu kusafirisha mali za wizi vingeweza kuthibitiwa .

"Wapo baadhi ya watu wanalalamikia uwepo wa askari wa usalama barabarani ....ila kwa sehemu kubwa kazi zinazofanywa na askari hao zinapaswa kupongezwa kwani bila uwepo wao umeendelea kulisaidia Taifa kupunguza ajali za barabarani na kusaidia pia kukamatwa kwa mali za wizi kama hizo ."

Kwa upande vwake Sanga alisema kuwa pamoja na askari wa usalama barabarani mkoa wa Iringa kuendelea kulalamikiwa kwa kuwabana madereva ila bado utendaji wao wa kazi unasaidia kwa kiasi kikubwa kuthibiti ujangili na ajali hivyo bado alitaka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua waharifu ambao wanasafiri katika mabasi hayo ya abiria .

Mtuhumiwa huyo wa ujangili akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kukamatwa na vipande hivyo vya pembe za ndovu alisema kuwa mzigo huo alikuwa ametumwa na mmoja kati ya wafanyabiashara mjini Dodoma na kuwa hivyo alikuwa akiupeleka Dodoma kwa ajili ya biashara .

Hata hivyo hakuweza kutaja thamani ya mzigo huo japo alisema kuwa alilazimika kutumia mabegi hayo matatu kupanda vipande hivyo vya pembe za ndovu ambazo ametokana nazo katika hifadhi ya Katavi mkoani katavi kama njia ya kukwepa kukamatwa na polisi.

Askari waliomkamata mtuhumiwa huyo waligoma kuzungumzia tukio hilo kwa madai kuwa wao si wasemaji wa juu ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa huku kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Evarist Mangalla alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema taarifa kamili ya tukio hilo ataitoa baada ya kufikishwa ofisini kwake.

No comments:

Post a Comment