Friday, February 24, 2012

MAZOEZI......MAZOOOEEEZIII:

Kama kawaida yetu, wazee wa kazi, wazee wa mazoezi ya vioungo na michezo. Jana, alhamisi, tulikusanyika tena katika viwanja vya michezo vya BOT Training Institute - Mwanza katika kuendeleza lile 'libeneke' la michezo na mazoezi ya viungo, ilikuwa safi sana japo na uchache wetu.
D-Tyming Malosha akijaribu kujaza jaza mpira wa kuchezea Volleyball pembeni akiwa na dada Naima.
Aah ahh, dada Naima wee, dada pekee wa michezo.
Aah..!!, Mzanziberi wee, michezo kwa afya bana.
Solis Maanya Ally akipiga shuti kumshinda Mzanziberi.
Caris katikati (kwa football paleee).
Caris kwa chenga za maudhi, balaaaa.
Pande kwa Mzanziberi paleeee.



Aahh, Wapinzani wetu walikuwa wepesi sana tuliwafunga magoli 3-0.
Tukaingia kwa basketcot, aerobics zikaendelea.
Sana tu.


 Twasonga.


 Mwili haujengwi kwa tofali na wala haulindwi na mmasai bali kula vizuri na kushiriki katika mazoezi mara kwa mara.
 Tukahamia kwenye Tai-Chi, si mchezo hapa kaaazi tu.

 This is Tai-Chi.
Baada ya shughuli kukamilika, mtaani kidogo. Hakuna kupanda panda gari hapa, tumezaliwa tutembee.

NB: Kwa wale watakaopenda kushiriki nasi, ratiba ya mazoezi haya ya viungo na michezo imebadilika, awali ilikuwa kila siku ya Jumatatu na Alhamisi ila kuanzia jana ni kila siku za kazi (Jumatatu-Ijumaa), mambo yamezidi kunoga. Karibuni saaaana tujumuike.

No comments:

Post a Comment