Tuesday, January 24, 2012

WASHINDI WA TUNZO MBALIMBALI ZA ZIFF - 2011/2012:


Kanumba akipokea tunzo ya Best actor kutoka kwa Mr.Danny wa ZIFF, "Shukrani zangu za dhati kwa majaji,shukrani kwa waandaaji,shukrani kwa mashabiki wangu wa roho na kweli,shukrani kwa walionipigia kura na kunipendekeza,zaidi ya yote sifa na utukufu nitaendelea kumrudishia mfalme wa maisha yangu YESU KRISTO na MUNGU BABA maana yeye ndiye aliyeniahidi ktk Biblia yake takatifu kuwa nikimtumaini yeye atanifanya kuwa kinara na si mkia tena atanifananisha na mlima Sayuni sitoteteleka milele, waigizaji wazuri tupo wengi ila imempendeza Mungu nichukue mimi tuzo hii kuwasilisha uzuri wa wengi tulionao". Alisema Kanumba.
 JB alichukua tuzo ya filamu bora (Senior bachelor) hongera sana kaka yangu nakumbuka, binafsi, baada ya kutizama filamu hii nilikupigia simu kukupongeza hasa kwa stori na uchezaji wako,mwandishi Vincent Van Goh anasema...appreciate people so that one day u ll be appreciated,if u don,t do that no one will appreciate you,,
Hiyo ilikuwa ni tuzo ya msanii bora chipukizi.....
Kambarage akipokea tuzo ya Steps Entertainment co Ltd kama kampuni bora ya usambazaji wa movie.
The great akipokea tuzo nyingine ya BEST FILM IN SOUND (DEVIL KINGDOM) hii ni ile aliyocheza na nguli Ramsey toka Nigeria, "Filamu zenye ubora huu wa sauti zipo nyingi ila imempendeza Mungu Filamu yangu kuchukua tuzo hii kuwakilisha ubora wa sauti katika filamu zetu tulizonazo". Alisema Kanumba.
Issa Musa (Cloud) akichukua tunzo ya BEST DIRECTOR,Hongera sana kaka yangu kumbuka Chanda chema siku zote huvikwa pete.
Picha ya pamoja ya washindi wote wa tunzo waliokuepo jana maisha club......
Interview ya Cloud mara baada ya tunzo nae kama kawa alilia na bodi ya filamu.....
Kwa niaba ya Ray ambaye hakuwepo ukumbini, Kanumba alimchukulia tunzo yake ya THE MOST INFLUENTIAL ICON.




Maneno ya mwisho ya Kanumba mara baada ya zoezi la upokeaji wa tunzo yalikuwa ''Hata tukiwa na uwezo wa kuhamisha milima kama hatupendani ktk tasnia ni kazi bure,kile kilicho moyoni ndio kioneshe usoni na sivinginevyo kama wanichukia moyoni basi onesha usoni na kama wanipenda moyoni basi onesha usoni na si vinginevyo,Isiwe moyoni wanichukia alafu usoni wanichekea,Hii sanaa ni karama tuliyobarikiwa na Mungu tuitumie vyema kwa ajili ya utukufu wake maana ipo siku atatuuliza na kutudai,kama katupa bure basi anao uwezo wa kutuny'ang'anya pia''soma Wakorintho uone jinsi Mungu alivyogawa karama hizi na ni kwanini katugawia". Alihitimisha Kanumba.

The great mara tu baada ya kuingia club Maisha na kupita red carpet interview mbalimbali zilianza kama unavyoona hapo.Hongera sana waandaaji wa tuzo hizi ZIFF.Hongera Mr,Danny.Kauli mbiu ya tuzo hizi na red carpet ilikuwa kuhimiza jamii kununua kazi ORIGINAL za movie hapa nyumbani na si FEKI,lakini pia kuhimiza uzalendo wa dhati kabisa katika sanaa ya nyumbani hususani filamu.
Odama na Maya nao walikuepo hapa maisha club.
Movie stars mbalimbali waliitumia siku hii kama siku yetu maalumu.
JB akihojiwa hapo ktk red carpet.,Pia akilia sana na bodi ya filamu juu ya mambo wanayotaka yafanyike ktk tasnia.
Irene Uwoya, msanii na Mzee Magali walikuepo.
Richie Richie, Monalisa na Mama Natasha walikuepo.....
Hapo Kanumba akitoa maoni yake juu ya sheria mpya zilizotolewa na Bodi ya filamu nchini ambapo karibia wasanii wote nchini wamezipinga na kuzikataa maana zinaua tasnia hii ambayo tumepata shida sana kuifikisha hapa ilipo, "Leo watu wachache tu bila kufanya uchunguzi wa kina wanaweka vitu ambavyo ni ndoto kwa wasanii sie tunaoibiwa kazi zetu na tusio na soko maalumu kuzitimiza."
Interview ikiendelea hapo.......
Tino, Dinno, Mzee Chilo, Baby Madaha walikuepo...
Irene Uwoya katika interview lakini pia nae hapo akishangaa hizi sheria za bodi ya filamu,,,,
Pilipili Entertainment nao walikuepo...
Big boss, Mr.Dilesh wa Steps entertainment akiteta jambo na Richie Richie...
Edwin Kileo mzee wa Subtitle alitaka kuhakikisha kiatu cha Kanumba kama kweli ni CL toka Paris-Ufaransa naye akamhakikishia...ahhahah Wazee wa pamba mnajua hii manenoooo,,,,?????
Furahia Swahili movie na nunua kazi original na si feki na kuwa mzalendo wa kazi za nyumbani kumbuka mcheza kwao hutunzwa na mkataa kwao mtumwa.

No comments:

Post a Comment