Akizungumza na chanzo chetu, juu ya harakati zake za mwaka 2012, msanii huyo alisema amekuwa katika maandalizi ya filamu lakini kubwa lililomfurahisha ni kupata bahati hiyo kama msanii kutoka Tanzania.
“Kuna kipindi nilikuwa nawasiliana na ‘Mercy’, kwa njia ya mtandao na nilikuwa nazungumza naye mambo mbalimbali kuhusu sanaa hivyo akanieleza kuwa akiwa anatatengeneza filamu yake ataweza kunitumia,” alisema.
Najma alisema mbali na kwenda nchini Nigeria pia yupo katika maandalizi ya filamu yake ambayo itakuwa inaelezea mafuriko yalitokea mwishoni mwa mwaka jana ambayo yalisababisha watu wengi kukosa makazi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment