Tuesday, January 24, 2012

MWENYEKITI WA MFUKO WA BODI YA BARABARA, DKT JAMES WANYANCHA, AFANYA UKAGUZI WA MAENDELEO YA UKARABATI WA ENEO LA DARAJA LA MBEZI KATIKA BARABARA YA MOROGORO ILIYOHARIBIWA NA MAFURIKO:

Mwenyeki wa Mfuko wa Bodi ya Barabara James  Wanyancha akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (pichani hawapo) kuhusu maendeleo ya ukarabati wa eneo la daraja la Mbezi katika barabara ya Morogoro (Morogoro road (Mbezi) iliyoharibiwa na mafuriko ya mwaka jana, ambapo mfuko wake umetoa fedha za dharura zaidi ya shilingi bilioni tano (5b/-) zilizoombwa na mkoa wa Dar es salaam kwajili ya kusaidia ukarabati.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa barabara, Dkt James Wanyancha (kushoto), pamoja na Mhandisi Julius Ngusa kutoka ofisi ya Tanroads (wa pili kulia) wakimsikiliza Mhandisi Ndekumana wa Tanroads(kulia) kuhusu uharibifu wa daraja la Tabata Kinyerezi Mkoani Dar es Salaam lilioharibiwa na mafuriko mwisho wa mwaka 2012.ambalo lipo kwenye ukarabati.
Mafundi wakiendelelea na ukarabati huko barabara ya morogoro eneo la mbezi.
Fundi akiwa kazini daraja la Salender Bridge.
Uharibifu wa mazingira kwenye daraja la boko watu wakiendelea kuchimba mchanga.
Ukarabati wa eneo la daraja la Matosa huko Goba katika wilaya ya Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam ambalo Mwenyekiti wa Mfuko wa Bodi ya Barabara Dkt. James  Wanyancha (hayupo pichani ) alikagua maendeleo ya ukarabati.

No comments:

Post a Comment