Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikisikia neno China China, hili linamaanisha kila kitu, siku za hivi karibuni neno hili limehusishwa sana na ufake,kutodumu nk. Binafsi nikiwa fans wa made in China, iwe kwa kukosa njia nyingine au urahisi ninaweza kusema machache ambayo nadhani yatakuwa na msaada kwa wengine. Nikiwa Mtanzania niliyeishi China kwa miaka zaidi ya sita, ninapenda kushare nawe mambo machache ambayo wafanyabiashara hawawezi kukuambia kuhusu Made In China.
Nikiwa barabarani kwenye pikipiki simu yangu ilidondoka, nikasikia mchina akiita "simu imedondoka" nikasimama na kuangalia kumbe ni simu yangu. Kwa bahati mbaya ilikuwa katikati ya barabara hivyo sikuwa na cha kufanya zaidi ya kuiangalia ikikanyagwa na basi la abiria, baada ya lile basi kupita taa nyekundu ikawaka na nikakimbia kuangalia masalio ya simu, nikaona kioo kimevunjika, nilipoishika nikaona ukiondoa kioo hakuna kingine. Niakajaribu kupiga simu ikawa inaita bila matatizo. Kesho yake nikaipeleka kwa wenyewe Nokia, wakaiangalia wakasema ukiondoa kioo hakuna tatizo. Ni kweli nimebadirisha kioo na sasa inadunda bila wasi.
1. Kuna Vitu China ni Ghali kuliko hata Tanzania.
Unaweza kusema kivipi, ila ni kweli, ukiwa Uchina na unataka kupata kitu chenye ubora mzuri, ni dhahiri unatakiwa kulipia zaidi. Binafsi nimekuwa nikipokea simu nyingi mno toka nyumbani wakitaka kunitumia pesa niwanunulia komputa nk. Ukienda sokoni kompyuta ya kawaida ambayo ni bora inaanzia yuan 2000, tena hiyo ni ile ya kiwango cha chiiini kabisa, ila ukiipeleka kwenye dola ni kama mia tatu kadhaa, ukijumlisha na utumaji mpaka inafika nyumbani ni kama dola mia tatu na nusu au mia nne. Hapo ndio unapata kompyuta ya kawaida mno kitu ambacho kwa mtanzania wa kawaida lazima aone ghali kwani akienda sokoni anaona DELL kibao kwa laki tanotano.2. China kuna bei tatu.
Kama umewahi kufika Uchina ni dhahiri utakubaliana nami, ukienda dukani unaulizwa unataka ipi, Hao(nzuri), Yiban(Ya kawaida) Shuihuo(Dump aka fake). Kwenye kila kundi ubora ni tofauti,ingawa kwa macho zote zinaonekana sawa. Pindi ununuapo ni lazima uhakikishe unapata kulingana na mapenzi yako. Hongera kwa wafanyabiashara WENGI wa Kichina ni kuwa, atakuambia. Hii ni nzuri na hii ni mbaya. Pia hata kwenye hiyo nzuri nayo kuna makundi yake humo ndani.hehe. Hivyo kabla hujanunua ni lazima ujue nini unataka na lazima muelewani na muuzaji.3.Kitu cha 100Yuan si cha 80Yuan.
Kwa wale waliowahi kukutana na Watanzania au wageni kadhaa walioishi Uchina kwa miaka mingi watakubaliana nami, jinsi muda uliokaa China unavyooongezeka ndivyo uwezo na ari ya kupatana bei inavyokwisha. Binafsi ni mara chache mno ukaniona ninapatana bei. Hii ni kwa sababu tayari wanafahamu hili. Kuna siku niliambatana na dada mmoja kununua simu, alipofika kule simu aliyopewa ilikuwa ni ya mia nane, akazidi kupatana (pianyipianyipianyi) basi mwisho yule mchina akakubali, yule dada akasema nachukua hii, mchina aliwaka kama kawekwa petroli. Akibwabwaja "haiwezekani,hii ni ghali nk) mwisho ikabidi mdadaa aongeze pesa.4. Kuna maduka yanayojulikana kwa ufeki na ubora.
Kila sehemu wana mila na tamaduni zao, ukiwa China, kama unataka kupata kitu chenye hadhi na ubora mzuri basi unashauriwa ukanunue kwenye maduka makubwa, kwa mfano unataka kununua TV ya nyumbani basi nenda kwenye maduka kama ya Sunning, Gomao,carrefour nk kwani mengi ya maduka haya yana mkataba wa ubora na bei na serikali. Kuna kipindi Carrefour walipandisha bei kiholela kwa baadhi ya vifaa vyao, walipigwa faini na ikawacost mno. Binafsi mwaka jana nilinunua simu ya mkononi "Nokia", wiki iliyopita kilitokea kitendo kilichonisukuma kuandika makala hii.Nikiwa barabarani kwenye pikipiki simu yangu ilidondoka, nikasikia mchina akiita "simu imedondoka" nikasimama na kuangalia kumbe ni simu yangu. Kwa bahati mbaya ilikuwa katikati ya barabara hivyo sikuwa na cha kufanya zaidi ya kuiangalia ikikanyagwa na basi la abiria, baada ya lile basi kupita taa nyekundu ikawaka na nikakimbia kuangalia masalio ya simu, nikaona kioo kimevunjika, nilipoishika nikaona ukiondoa kioo hakuna kingine. Niakajaribu kupiga simu ikawa inaita bila matatizo. Kesho yake nikaipeleka kwa wenyewe Nokia, wakaiangalia wakasema ukiondoa kioo hakuna tatizo. Ni kweli nimebadirisha kioo na sasa inadunda bila wasi.
No comments:
Post a Comment