Mwandishi mkongwe wa habari Tanzania na Mtangazaji Marehemu John Ngahyoma.
MTANGAZAJI wa muda mrefu wa iliyokuwa Redio Tanzania Dar esSalaam RTD na baadae Shirika la Utangazaji Tanzania (SHIUTA)MarehemuHalima Mkuchika
---
Halima nae Ngahyoma.
Mola twakushukuru, kwahii yako rehema,
Mola wewe ni nuru, Mja wetu wa Karima
Mola umetunusuru, kwa nyingi dhahama.
Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.
Mola upe amani Halima, dada yetu maridhawa
Mola umpumzishe daima, mtangazaji wa dawa,
Mola ulimpa rehema, mpirani alikuwa muruwa,
Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.
Ulipomwita Ngahyoma, hakusita kuitika,
Leo katuacha nyuma, nyumbani na Afirika,
Sikioni bado vuma, utangazaji wake hakika,
Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.
Pole wanahabari, Tanzania na dunia,
Msijione wahatari, Mola anapowachagua,
Tujipange misitari, ibadani kuwaombea,
Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.
Kazi ya mola timilifu, daima haina makosa,
Tuwahifadhi nadhifu, tusamehe waliokosa,
Mavazi yawe ya sufu, tuwavishe wao sasa,
Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.
Wanalia wanafamilia, Wahalima na Ngahyoma,
Wahariri wanawalilia, hakika imewachoma,
TBC na BBC walia, wapendwa wametuhama,
Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.
Majonzi yamenifika, Mroki nagugumia,
Moyo imenishtuka, habari ziliponifikia,
Hakika tutawakumbuka, Halima na Ngahyoma,
Kaditama natamatia, Mroki nawakimbia,
Mola atawakumbatia, wafiwa nawaambia,
Hakika nitawafuatia, Mola ataponiambia,
Mola uwarehemu, Halima nae Ngahyoma.
Mroki Mroki “Father Kidevu”
0755373999/0717002303
UKONGA-DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment