Friday, November 18, 2011

KILA KITU NYERERE, NYERERE,NYERERE:

ILIKUWA MAJIRA YA SAA MBILI ASUBUHI NILIPITA KIJIJI CHA NYAMISWI KATA YA KOME KATIKA KITUO CHA AFYA KOME WILAYA YA SENGEREMA NA NIKAKUTA UMATI MKUBWA WA WANAKIJIJI WAKISUBIRI HUDUMA BILA WAHUDUMU, MAANA KITUO KILIKUWA KIMEFUNGWA NA FUNGUO ZIKIWA NA MGANGA MFAWIDHI AMBAE MPAKA MAJIRA YA SAA TANO KASORO ROBO HAKUONEKANA KITUONI NA KWA KIASI KIKUBWA WAGONJWA WENGI WALIKATA TAMAA NA KUAMUA KUONDOKA. ALIYELALA CHINI NA MBELE YA MLANGO MKUU WA KITUO HICHO NI MAMA AMBAE NILIAMBIWA AMEVUJA DAMU KWA MUDA MREFU BAADA YA MIMBA KUHARIBIKA NA BAADA YA KUONA MGANGA HATOKEI WALIANZA KUTAFUTA MSAADA WA USAFIRI KWENDA WILAYANI, KUMBUKA HAPO NI KISIWANI NA MPAKA WAFIKE KIVUKONI NI MWENDO MREFU KIDOGO INGAWA NIKIWA HAPO NILIONA GARI MOJA LENYE NAMBA ZA DFP SIJUI KAMA LILITOA MSAADA HATA WA KUMFIKISHA KIVUKONI

NILIUMIA SANA MAANA KULIKUWA NA WAGONJWA WENGI NA WAHUDUMU WAWILI WASIO NA FUNGUO WALA VITENDEA KAZI
Na Rashid Kindole.
Habari kwa hisani ya: http://www.mjengwablog.com/

No comments:

Post a Comment