Thursday, November 24, 2011

FILAMU YA CPU KUANZA KUONESHWA RASMI IJUMAA TAREHE 25 NOV 2011 @ CENTURY CINEMAX-MLIMANI CITY:

Evans Bukuku akitoa maelezo kuhusu filamu ya CPU, Mkurugenzi wa Haakneel, Godfery Mahendeka (Kushoto) na Director wa filamu hiyo Karabani (Kulia).
Sauda Simba (Kushoto), mhusika mkuu katika filamu hiyo.
 

Director wa Filamu ya CPU Karabani akitoa maelezo na Steven Sandhu mhusika mkuu katika filamu ya CPU.
Evans Bukuku akionyesha Poster ya Filamu ya CPU.
-- 
Ile filamu ya C.P.U ambayo imekuwa ikisubiriwa na Watu wengi hatimaye mwisho wa wiki hii itaweza kuzinduliwa na kuoneshwa rasmi kwa wapenzi wa tasnia ya filamu.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa filamu ya C.P.U bwana Evans Bukuku alisema kuwa “Filamu ya C.P.U kwa mara ya kwanza itaoneshwa  hapo Ijumaa tarehe 25 Novemba 2011 kuanzia saa 1 na dakika 45  jioni katika ukumbi wa Sinema wa mlimani city century cinemax, kisha itaendelea kuoneshwa kwa wiki nzima muda kama huo mpaka mnamo tarehe 1 Disemba 2011.
 
Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa wapenzi wa tasnia ya filamu na watanzania wote kwa ujumla  kwenda kupata kujionea kazi ya ubora wa hali ya juu ambayo imefanyika hapa Tanzania.Kwa wale watakaopata nafasi ya kuitazama Filamu ya C.P.U hakika watathibitisha hili.
 
Akizungumzia kwa ufupi juu ya Filamu hii Bw. Bukuku alisema, “ filamu ya C.P.U imetengenezwa na kampuni ya Haak neel  kwa ushirikiano na Wegos Works Production ikiwa imeandikwa na Novatus Nago na kuongozwa na Karabani huku watayarishaji wakuu wakiwa ni Prof. Martin Muhando na Bw Godfrey Mahendeka. CPU ni aina ya hadithi ya kipelelezi yaani ‘Investigatory story’ ikiwa  inazungumzia kitengo kilichoundwa kwa ajili ya kufuatilia na kutatua matatizo yanayowapata watoto. Hivyo Maria Isabela (Sauda Simba) anateuliwa na serikali kuongoza timu  hiyo,  katika hilo inabidi awashawishi watakao msaidia ambao ni Alex Kibera(Nkwabi Juma) jambazi anayetumikia kifungo cha miaka 30 jela, David Kifati(steven Sandhu) mtaalamu wa kompyuta na kijana mwenye uelewa mkubwa ambaye anatoka katika familia bora na anayependa anasa, pia kuna Rehema Mlaki (Subira Wahure) akiigiza kama msichana anyefanya kazi ya uwakili wa kujitegemea.
 
Baada ya kufanikiwa kuwashawishi wanaanza kazi ya kwanza ambayo kiujumla ni yenye misukosuko na inayohitaji umakini wa hali ya juu kwa kuwa ni ya hatari sana  hasa wanapokabiliana na mtu kama Jibaba(Mobby Mpambala) mmiliki wa danguro kubwa hapa jiji na mzoefu wa biashara haramu.hapo ndipo utapata kuona mikiki na ufanisi uliooneshwa na waagizaji takribani 180. Filamu ya CPU ikiwa imetengezwa hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo tofauti zaidi ya 30.
 
Lugha iliyotumika katika filamu hii ni Kiswahili lakini pia lugha ya kiingereza imetumika kama “subtitles”. Umri wa kutazama filamu hii ni kuanzia miaka 13.Kiingilio  filamu ya C.P.U ni sawa na kiingilio cha kawaida cha  Century Cinemax 
Mpaka kufanikisha tukio hili tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono tangu mwanzo,  East Africa Radio na East Africa Television, I-Noch Company Limited , waandishi wahabari wote kwa ujumla , baadhi ya Taasisi za kiserikali, mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali hasa yanayohusika na masuala ya watoto na watu mbali mbali.
Unaweza kuanza kufanya booking ya Ticket yako kuanzia sasa kupitia namba  
0715 246362 
0753 246362
 
Kwa maelezo na taarifa zaidi juu ya filamu ya CPU unaweza kupata kupitia vyombo mbali mbali vya habari pia unaweza kufuatilia zaidi kupitia tovuti ya http://www.cpu.co.tz/ au http://www.filamucentral.co.tz/

No comments:

Post a Comment