Dr. Rebeca Cammer akimvalisha miwani mtoto Henry Abel anayesoma Shule ya Lake View.
Alfred Kapole Mwenyekiti wa chama cha maalbino mkoa wa Mwanza kwa upande wake aliiomba Selikali kutoa msisitizo na kipaumbele kwa walemavu wa ngozi mashuleni wasihusishwe na kazi za juani ikiwa ni pamoja na kujipanga mstarini kwa nia ya kuwanusuru na kansa ya ngozi.
Dr. Rebeca Cammer akimuuliza maswali mtoto Maisha Msobi juu ya uono mara baada ya kuvalishwa miwani maalum kwa macho kuona taswira za mbali.
Dr. Rebeca Cammer akijaribu kuona kama zoezi limefanikiwa kwa uono wa mtoto Masanja mara baada ya kukabidhiwa miwani ya macho itakayomsaidia kuona mbali ubaoni wakati wa masomo darasani.
Wengine mbali na kupewa miwani walipewa lensi maalum kwaajili ya kusomea.
Kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa nguvu ya macho ya mtoto huyu ajulikanaye kwa jina la Thabitha alikabidhiwa miwani aina mbili kutokana na vipimo alivyofanyiwa vya macho kugundua zitakazo msaidia kuona mbali na karibu.
Vilevile kulikuwa na kifaa hiki maalum kilicho na uwezo kama darubini kwaajili ya kuona mbali.
Vipimo vikiendelea toka kwa Dr. Rebeca.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa shirika hilo nchini Tanzania Vick Mtetema amesema kuwa shirika lake limefarijika sana kukamilisha ahadi hiyo lililoiweka mwezi wa sita mwaka huu kama sehemu ya kuwawezesha katika elimu wanafunzi wenye uono hafifu ambao wamekuwa wakitengwa na wamekuwa wakitaabika kuona katika kujisomea au wakati wa mafunzo darasani.Watu wenye ulemavu wa ngozi wanamatatizo mawili makubwa yanayo wakabili ikiwa ni pamoja na kansa ya ngozi ambapo hulazimika kuvaa mashati marefu na kofia, pamoja na tatizo la uono hafifu ambalo suluhisho lake ni kupatiwa miwani au vifaa maalum kukabiliana na tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment