Friday, July 1, 2011

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAKIWA MALABO IQUATORIAL GUINEA KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO WA 17 WA UMOJA WA AFRIKA:

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na baadhi ya wakuu wengine wa nchi za Umoja wa Afrika AU wakimpongeza Rais mstaafu wa Brazil Lula Da Silva kwa hotuba yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi za AU uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sipopo,jijini Malabo,Equatorial Guinea jana asubuhi.Hotuba hiyo ya kusisimua ilitilia mkazo kwa nchi za Afrika kushirikiana ili kujiletea maendeleo na kuepuka misaada yenye masharti inayolididimiza bara la Afrika katika lindi la umaskini.
 Mke wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, akishiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Umoja wa Afrika unaofanyika jijini Malabo, Equatorial Guinea.
Rais Jakaya Kikwete akishiriki kupanda mti wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU) katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta, Malabo.

Note: To post a comment:
Click 'comment',write your comment in the comment pad,THEN (Select Anonymous profile to hide your name OR Name/URL profile to disclose your name ie Name: (Write your name) and URL: (This is optional)) THEN Click 'Post comment',type the word shown for verification THEN Click 'Post comment'.

No comments:

Post a Comment